Mradi wa maji wa Mwanga – Same – Korogwe uko vizuri

0
196

Serikali imewaondoa hofu wananchi wa wanaohudumiwa katika mradi wa maji wa Mwanga – Same – Korogwe na kusema kuwa mradi huo uko katika kiwango bora cha utekelezaji wake.

Naibu waziri wa Maji Mhandisi Merryprisca Mahundi amewatoa hofu wananchi hao wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum, Mwantum Zodo aliyetaka kujua mwenendo wa ujenzi wa mradi huo.

Mhandisi Mahundi amesema, mradi huo unaendelea vizuri na uko katika hatua nzuri za kuwahudumia wananchi wa wilaya za Mwanga, Same na Korogwe.