Kagera Sugar na Dodoma jiji hakuna mbabe

0
1153

Mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara umechezwa leo kwa kuwakutanisha wana supa nkurukumbi Kagera Sugar dhidi ya Walima zabibu Dodoma jiji, mchezo uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Kagera walikuwa wenyeji wa mchezo huo ambapo wameshindwa kutumia vema kiwanja cha nyumbani kupata alama tatu. Kila timu inafikisha alama mbili baada ya wote kupoteza michezo miwili na kutoa sare michezo miwili.