Magoli mawili ya mshambuliaji kutoka Zambia Moses Phiri, yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 2-0 pia kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita jijini Lilongwe nchini Malawi, Phiri akifunga moja na lingine, Nahodha, John Bocco.
Sasa vigogo hao wa Tanzania watakutana na mshindi wa jumla kati ya Primiero de Agosto ya Angola ama Red Arrows ya Zambia katika hatua inayofuata.
Mechi ya kwanza Agosto walishinda 1-0 nyumbani na leo watakuwa ugenini nchini Zambia.