Wafanyakazi Afrika Kusini waandamana

0
921

Vyama vya Wafanyakazi nchini Afrika Kusini vimeongoza maandamano makubwa katika mji wa Johannesburg, maandamano yenye lengo la kupinga sekta binafsi kupunguza wafanyakazi.

Sekta ya madini nchini Afrika Kusini ndiyo imepunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa.

Raia wengi wa Afrika Kusini wamesema kuwa wanaitegemea sekta ya madini kwa ajili ya ustawi wa maisha yao, kwa kuwa inatoa ajira kwa watu wengi.

Vyama vya Wafanyakazi nchini Afrika Kusini pia vinaishinikiza serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua kuwasaidia wafanyakazi ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kupitia sekta ya madini kukuza uchumi wa Taifa hilo.