RC Makalla : Mafunzo ya Jeshi yanasaidia vijana

0
315

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, amesema mafunzo ya jeshi kwa mujibu wa sheria yanasaidia vijana kujifunza mambo mbalimbali yenye tija katika Taifa.

RC Makalla ameyasema hayo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya jeshi kwa mujibu wa sheria yaliyofanyika katika kambi ya CUJKT Kimbiji iliyopo Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake Mkuu huyo amewahimiza wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele kuona umuhimu wa mafunzo ya JKT mujibu wa sheria kwakuwaruhusu vijana wao kujiunga na mafunzo hayo ili wajengewa uwezo katika shuguli za uzalishaji Mali na uzalendo Kwa Taifa.

Aidha amewataka vijana waliohitimu mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulizi na usalama.

Jumla ya vijana 685 wamehitimu mafunzo ambayo yalianza julai 17 mwaka huu katika Chuo Cha Uongozi JKT Kimbiji wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.