Mtambo mkubwa wa kuhudumia makasha wawasili

0
309

Meli iliyobeba mtambo mkubwa wa kuhudumia shehena ya makasha imewasili katika bandari ya Mtwara, ikiwa pamoja na meli nyingine maalum iliyobeba vifaa vya kufungia mtambo huo wenye uwezo wa kushusha makasha kwa umbali wa hadi mita 45 kutoka kwenye gati.
 
Akishuhudia kuwasili kwa meli hiyo mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema, serikali bado inaendelea kuiongezea uwezo bandari ya Mtwara, ili kuhakikisha inafanya kazi kulingana na uwekezaji uliofanyika.

Amesema meli hiyo imebeba mtambo mmoja kati ya mitatu iliyoagizwa na serikali kwa ajili ya bandari za Dar es Salaam na Mtwara, ambayo imegharimu shilingi bilioni 85.
 
Kaimu meneja wa bandari ya Mtwara Mhandisi Norberth Kalembwe amesema, bandari hiyo kwa sasa ina uwezo mkubwa wa hudumia meli pamoja na mizigo, hivyo wafanyabiashara wanakaribitishwa kuitumia.