Walipwa fidia baada ya kusubiri miaka 22

0
231

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) imewakabidhi fedha ya fidia wananchi hamsini waliokuwa wanaidai mamlaka hiyo, kutokana na eneo lao ambalo serikali ililichukuwa miaka 22 iliyopita kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji.

Wananchi hao wamekabidhiwa fedha hizo na kutakiwa kuondoka katika eneo la Mangamba Juu manispaa ya Mtwara, Mikindani ndani ya kipindi cha siku 90.

Eneo hilo lilichukuliwa mwaka 2001 na MTUWASA kwa ajili ya ujenzi wa chujio la maji, lakini wananchi waligoma kuondoka wakidai fidia bila mafanikio.

Mapema mwezi huu Rais Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi milioni 816.78 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi hao, ambapo kwa sasa wanatakiwa kuondoka ili kupisha utekelezaji wa mradi huo wa maji.