Serikali yawatoa hofu wananchi kuhusu usalama wa samaki

0
181

Serikali imewatoa hofu wananchi kuhusiana na usalama wa samaki wanaovuliwa katika ziwa Viktoria, na kusema kuwa mengi yanayosemwa ni nadharia ambayo haina ukweli wowote.

Naibu wazri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amelieleza bunge jijini Dodoma kuwa, samaki wanaovuliwa na kusafirishwa kwenye maeneo mbalimbali nchini ni salama na sio kweli kuwa wanahifadhiwa kwa kutumia dawa za kuhifadhia maiti.

Ulega amesisitiza kuwa samaki wote wanahifadhiwa kwa uangalizi maalum na kwamba sio rahisi kutumia dawa hizo kwenye uhifadhi wa samaki wanaovuliwa ziwa viktoria.

Naibu waziri Ulega alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti maalum Cecilia Pareso.