Mkutano wa haki za binadamu waendelea Geneva

0
683

Mkutano wa 51 Baraza la Haki za Binadamu umeendelea leo katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo Geneva, nchini Usiwsi.

Katika Mkutano huo Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Eliamani Sedoyeka ambapo vikao mbalimbali vya kuzungumzia nchi katika masuala ya athari za Uviko-19 na Haki za Maendeleo.

Masuala mengine yaliyozungumzwa ni pamoja na juhudi zilizowekwa na Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha Watanzania wananufaika katika Haki za Maendeleo.

Maeneo mengine yaliyozungumziwa ni pamoja na Elimu Bure kwa wanafunzi wa Sekondari, Sensa na mpango mkakati wa Maendeleo baada ya Uviko 19.