Ziara ya bodi ya TBC

0
211

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Stephen Kagaigai, leo imetembea ofisi za shirika hilo zilizopo barabara ya Nyerere na zile zilizopo Mikocheni mkoani Dar es Salaam.

Wakiwa TBC, wajumbe hao wamepata fursa ya kujionea namna vitengo mbalimbali vya shirika hilo vinavyotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Hivi karibuni waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye aliteua wajumbe saba wa bodi ya wakurugenzi wq TBC ambao ni
Tuma Abdallah, Amina Mollel, Cosmas Mwaisobwa, Innocent Mungy, Mwanjaa Lyezia, Dkt. Hidelbrand Shayo na Justina Mashiba.

Waziri Nape aliwateua wajumbe hao kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo ya Wakurugenzi wa TBC.