Wanamuziki wamlilia Godzilla

0
730

Wasanii mbalimbali wa muziki nchini wameendelea kutoa pole kufuatia kifo cha  Mwanamuziki wa miondoko ya Hip Hop nchini Golden Mbunda maarufu kama Godzilla aliyefariki dunia ghafla usiku wa Jumatano Februari 13 mwaka huu  nyumbani kwao Salasala jijini Dar es salaam.

Kwa sasa mwili wa Godzilla umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi  ya Lugalo.

Wakati wa uhai wake, Godzilla ametunga na kuimba nyimbo mbalimbali na atakumbukwa kwa nyimbo zake kama vile Nataka na Kingzilla.

Godzilla  pia alijizoelea umaarufu na mashabiki wengi kutokana na umahiri wake wa kuimba mashairi ya papo kwa papo  yaani Freestyle.