Tanzania na Genova kushirikiana

0
1058

Chemba ya wafanyabiashara wa jiji la Genova nchini Italia imetia saini mkataba wa makubaliano na chemba za wafanyabiashara, viwanda, Utalii, biashara na kilimo za Tanzania Bara na Zanzibar.

Utiaji saini wa mkataba huo uliofanyika katika jiji hilo umeshuhudiwa na balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo, Rais wa chemba hiyo katika jiji Genova, Luigi Attanasio, Rais wa chemba ya wafanyabiashara Tanzania Bara Paul Koyi na Zanzibar aliyewakilisha ni Alhaji Ali Amour.

Chemba hiyo ya wafanyabiashara wa jiji la Genova nchini Italia ina wafanyabiashara zaidi ya elfu 70 ambao ni wazalishaji na wamiliki wa viwanda.

Mbali ya kutia saini mkataba huo, wafanyabiashara hao wa jiji la Genova wamethibitisha kuhudhuria kongamano la wafanyabiashara wa Italia na Tanzania linatotarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu kwa upande wa Zanzibar na tarehe 30 mwezi huu kwa upande Tanzania Bara.

Miongoni mwa mambo yaliyokubaliwa na pande hizo ni wafanyabishara hao kutembeleana, ili kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna ya kufanya biashara zenye tija.