Namungo yapata ushindi uwanja wa nyumbani

0
871

Klabu ya Namungo imeibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya wazee wa kupapasa Ruvu Shooting yenye maskani yake Mabatini mkoani Pwani.

Goli la Namungo limefungwa na Reliant Lusajo dakika ya 82 ya mchezo na kuwafanya ruvu kucheza mechi mbili mfululizo bila kupata ushindi.

Kwa matokeo hayo Namungo inafikisha alama saba huku Ruvu Shooting ikibaki na alama tatu.

Mapema leo katika uwanja wa Liti mkoani Singida walima zabibu kutoka Dodoma, Dodoma Jiji FC walikaribishwa na matajiri wa Alizeti Singida Big Stars ambapo hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi timu hizo ziligawana alama moja moja kwa kutoka suluhu Tasa.