Viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza, kilichotokea hapo jana akiwa na umri wa miaka 96.
Miongoni mwa viongozi hao ni Rais Xi Jinping wa China, Rais Joe Biden wa Marekani, Emmanuel Macron wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Italia Mario Drachi na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.
Tayari Marekani imetangaza bendera zake zote kupepea nusu mlingoti, kufuatia kifo hicho cha Malkia Elizabeth II.
Mfalme Charles III ambaye amechukua uongozi katika familia ya Kifalme nchini Uingereza amesema, kifo cha mama yeke ni pigo kubwa.
Malkia Elizabeth II ambaye alizaliwa mwaka 1926 amekuwa malkia wa kwanza nchini Uingereza kuongoza kwa kipindi kirefu ambapo ameshika wadhifa huo kwa takribani miaka Sabini.
Maelfu ya wananchi huko Uingereza wamaendelea kukusanyika katika Kasri la Buckingham, kuomboleza kifo cha malkia Elizabeth.