Ampa ujauzito binti yake ili asiolewe

0
127

Yeremia Chidaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kiteto mkoani Manyara, akituhumiwa kumpa ujauzito mwanae wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16.

Mshtakiwa amekiri kosa na kusema halikuwa kusudio lake kufanya hivyo na kwamba kitendo hicho kilitokana na kutotaka binti yake aolewe na kijana wa Kikamba.

Ameongeza kuwa alijaribu kuongea na mke wake na kumweleza matakwa yake ya mwanaye kutoolewa na Mkamba, jambo ambalo mama huyo hakuliafiki na kumjibu kuwa “basi wewe muoe” ndipo alipochukua uamuzi wa kufanya kitendo hicho.

Aidha, Baba huyo ameiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kutenda kwa kosa hilo.