Dkt. Ayub Rioba Chacha, mwongozaji wa kongamano NDC

0
141

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha ndiye mwongozaji wa kongamano la maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa ya chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kilichopo Kunduchi mkoani Dar es Salaam, ambapo mada kuu ni Uhuru wa Tanzania, Ujenzi wa Taifa, Usalama na Maendeleo.

Mzungumzaji mkuu katika kongamano hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye amewasilisha mada kuhusu Uhuru wa Tanzania, Ujenzi wa Taifa, Usalama na Maendeleo.

Unaweza kufuatilia matangazo haya kupitia TBC1 na mitandao ya kijamii Facebook, Instagram, Twitter na Youtube channel ya TBConline.

https://youtu.be/vCT-xgGxUJ4