Picha: Mazungumzo ya wakuu wa majeshi wastaafu

0
135

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali Davis Mwamunyage (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali Venance Mabeyo, katika ukumbi wa chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kilichopo Kunduchi mkoani Dar es Salaam, linapofanyika kongamano la miaka kumi ya chuo hicho.

Kongamano hilo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho, maadhimisho ambayo pia yatahudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan baadaye hii leo.