Serikali imeendelea na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato wakati wa kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kilichofanyika Bungeni jijini dodoma,
Aidha, kamati ya Bunge ilijulishwa kuwa majadiliano ya mikataba 39, iliyowahusisha wakandarasi wa mradi wa kusambaza umeme Vijijini (REA), awamu ya III mzunguko wa II, utekelezaji wake unaendelea kwa kuwa majadiliano hayakuwa yamewasilisha utekelezaji wa Miradi.
Pamoja na mambo mengine, kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti ilitaka kujua bei ya kuunganishia wateja wapya waliopo maeneo ya Vijijini kutofautiana.
Naibu waziri Byabato amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeunda timu ya wataalam ambayo iko kazini ili kuona uhalisia na hatimaye kuja na bei inayoendana na mazingira ya wananchi waishio katika maeneo ya Vijijini.