Kampuni ya Google inajitayarisha kukabiliana na wimbi la habari potofu kuhusu uchaguzi wa katikati ya muhula huko Marekani unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kudhibiti aina yoyote ya upotoshaji kwenye mtandao.
Kampuni hiyo imeeleza alhamis ya wiki hii kuwa njia itakazotumia ni kupitia kuweka habari za kuaminika na kuzionyesha kwa wingi na uwazi zaidi katika majukwaa yake yote kupitia kipengele chake cha utafutaji “search”na YouTube.
Hata hivyo kampuni hiyo imezungumza katika moja ya blogu nchini humo kuwa inapanga kuzindua zana mpya katika wiki zijazo ambayo inaangazia uandishi wa habari wa ndani na wa kikanda kuhusu kampeni za uchaguzi wa Marekani pamoja na utafutaji wa jinsi ya kupiga kura “how to vote” kwa lugha ya Kiingereza na Kihispania.
Hatua hiyo ya Google inakuja ikiwa zimepita siku kadhaa tangu jukwaa la Big Tech kuchapisha taarifa yenye kueleza utayari wa jukwaa hilo kupingana na uchaguzi huo jambo ambalo linaweza kuleta athari kwa uchaguzi huo.
Aidha mtandao wa Youtube ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Google tayari umeanza kuondoa video zinazohusiana na vuguvugu la uchaguzi wa Muhula wa kati ambazo zimetoa madai ya uwongo kuhusu uchaguzi uliopita wa 2020 kwa kukiuka sera zake, kampuni hiyo imeeleza kwenye chapisho lake.