Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tamasha la Kizimkazi ni nyenzo imara ya kuimarisha umoja na Mshikamano kwa wananchi wa Kizimkazi na Mkoa wa Kusini Unguja kwa ujumla
Majaliwa amesema Tamasha hilo litaenziwa na kuendelea kuratibiwa katika maeneo mengine ili kuendelea kudumisha na kuimarisha umoja upendo na Mshikamano kwa watanzania.
Aidha Waziri Mkuu amesema Rais Samia ni Rais Mwenye Upendo kwa Watanzania na kuwapongeza wana Kizimkazi kwa kumlea mtoto mwema
Katika Tamasha hilo Waziri Mkuu Kassim ametumia fursa aliyopewa kuzungumza na kutoa pongezi zake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kwa utendaji kazi wake pamoja na ushirikiano alionao kati yake na Rais Samia Suluhu Hassan