Marufuku kitimoto Makete

0
127

Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imepiga marufuku watu kuchinja nguruwe na kula nyama yake (kitimoto) kwa muda usiojulikana, kutokana na taarifa za uwepo wa ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Afisa Mifugo na Uvuvi wa wilaya ya Makete, Aldo Mwapinga ametoa taarifa hiyo kufuatia vifo vya nguruwe 21 wilayani humo.

“Kata ya Tandala kumeripotiwa dalili za ugonjwa wa homa ya nguruwe, kwa hiyo tunaendelea na jitihada za kuhakikisha tunashirikiana na watendaji kuanzia ngazi ya kata hadi vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea.” amesema Mwapinga

Amesema mbali na kupiga marufuku uchichaji huo wa nguruwe hasa katika kata hiyo ya Tandala, pia hairuhusiwi kutoa nguruwe kutoka kwenye zizi moja kwenda jingine.

Idara ya Mifugo na Uvuvi wilayani Makete
imewataka wakazi wa wilaya hiyo kuacha kufukua nguruwe waliofukiwa baada ya kufa (mizoga) na kuwachinja kisha kwenda kuuza nyama vilabuni nyakati za usiku.