Serikali kudhibiti mfumuko wa Bei ya vifaa tiba

0
228

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Afya kudhibiti mfumuko wa bei za vifaa tiba vya kutolea Matibabu Nchini.

Dkt. Godwin Mollel amesema hayo alipokutana na wazalishaji na washitiri mbalimbali wa bidhaa za afya wanaoshiriki maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yanayoendelea mkoani Dar Es Salaam.

Dkt. Godwin Mollel ameongeza kuwa kuna umuhimu wa Bohari za Dawa (MSD) kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kutoa huduma za matibabu kwa wananchi kwa bei nafuu na kuokoa fedha nyingi zinazotuniwa kununua vifaa tiba.