Ofisi za Tume ya Uchaguzi zachomwa moto

0
968

Ofisi za Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria katika jimbo la Plateau zimechomwa moto, zikiwa zimesalia siku Sita kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Polisi katika jimbo hilo la Plateau wamesema kuwa, moto huo umeteketeza kila kitu ambacho kinahitajika wakati wa uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na karatasi za kupigia kura na madaftari yenye majina ya wapiga kura.

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria imesema kuwa karibu maandalizi yote kwa ajili ya uchaguzi huo yalikua yamekwishakamilika katika jimbo hilo na kwamba kwa sasa haiwezi kusema kama kitendo hicho cha uchomaji moto ofisi ni hujuma au la.

Uchaguzi mkuu nchini Nigeria unatarajiwa kufanyika Jumamosi Februari 16 ambapo zaidi ya raia Elfu 84 wa nchi hiyo wamejiandikisha kupiga kura.