IJP Wambura: Tumeanza kutekeleza maagizo ya Rais

0
242

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IJP Camillius Wambura amesema Jeshi hilo limeanza kufanya utekelezaji wa maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa Jeshi hilo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo kwa Rais, IJP Wambura amesema, wameanza kuwachukulia hatua baadhi ya maafisa wa Jeshi hilo ambao wanakiuka miongozo iliyowekwa katika utendaji wao wa kazi.

IJP Wambura amesema, wamefanya uhakiki wa maabusu kwenye Magereza mbalimbali nchini na kugundua kuwa baadhi yao kesi zao hazikua na ushahidi wa kutosha na hivyo kuzifuta.

Amesema zaidi ya maabusu 4000 wamachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha wa kuendelea na kesi hizo.

“Kuhusu mahabusu, sisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama tumepitia majadalada na kugundua kuwa wapo ambao hawakuwa na kesi na hivyo kupitia ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa serikali kufutia kesi zao.

Ameongeza kuwa kwa sasa wanapitia utendaji kazi wa Askari wa Usalama barabarani ili kubaini wenye uwezo wa kuendelea kukaa barabarani ama kuhamishwa katika vituo vingine ndani ya jeshi hilo.

Kikao hicho cha siku tatu cha maafisa waandamizi wa Polisi wa makao makuu, makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi utaangazia mambo mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya jeshi hilo.