Yanga yapigwa faini

0
339

Klabu ya Soka ya Yanga, imepigwa faini ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) baada ya kukutwa na hatia ya kufanya makosa mawili.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeeleza kuwa Yanga imekutwa na makosa ya mashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani katika mchezo kati yake na Polisi Tanzania uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Agosti 16, 2022.

Kosa jingine la Yanga kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa mikupuo minne badala ya mikupuo mitatu, kosa lililofanyika katika mechi kati ya timu hiyo na Coastal Union uliopigwa Agosti 20, 2022 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.