WFP yaanza kununua mahindi Tanzania

0
1037

Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeanza kutekeleza mkataba wa kuuza Tani Elfu 36 za mahindi kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani( WFP).

Tani hizo zitasafirishwa kwenda kwenye nchi ambazo zina upungufu wa chakula Barani Afrika.

Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Kati,- Felix Ndunguru amesema kuwa tayari kazi kusafirisha mahindi hayo imeanza kutoka mkoani Dodoma na kupelekwa katika nchi hizo zenye upungufu wa chakula.

Amesema kuwa mkataba huo wa kuuziana mahindi umeanza kutekelezwa baina ya Tanzania na WFP baada ya serikali kujiridhisha kuwa nchi ina chakula cha kutosha.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji kutoka WFP, – Mahmud Mabuyu amesema kuwa wameamua kununua mahindi nchini Tanzania kutokana na mahindi hayo kuwa na ubora unaotakiwa.