WhatsApp kurejesha jumbe zilizofutwa

0
250

Programu tumizi ya whatsapp inayomilikiwa na kampuni ya Meta inaweka maboresho mapya yanayoruhusu watumiaji kurejesha jumbe zilizofutwa “delete for me” kwa mtumiaji aliyetaka ujumbe huo ufutike kwake peke yake na sio ujumbe uliofutwa kwa kila mtu “delete for every one”

Bado haijafahamika ni kwa muda gani baada ya kufuta ujumbe mtumiaji ataweza kurejesha ujumbe uliofutwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya WABetaInfo, Programu hii ya WhatsApp inayomilikiwa na kampuni ya Meta itatoa fursa kwa wasimamizi wa vikundi vya WhatsApp “group admin” kufuta ujumbe uliotumwa na mtu yeyote katika kikundi ambapo kipengele hiki kipya kimeanza kufanya kazi kwa majaribio kwa baadhi ya simu zenye programu ya whatsapp zinazotumia mfumo wa iOS.

Aidha inaelezwa kuwa, maboresho hayo yataendelea kufanyika kwa watumiaji wote wa simu zote zenye mfumo wa iOS na Android