Kamishna Jenerali wa Magereza aapishwa

0
127

Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Mzee Ramadhan Nyamka kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.

Hafla ya kumuapisha Kamishna Jenerali huyo wa Jeshi la Magereza imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.

Mbali na kumuapisha Kamishna Jenerali huyo wa Jeshi la Magereza, Rais Samia Suluhu Hassan pia amewaapisha Majaji 21 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni.