Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo amehudhuria ufunguzi wa mkutano wa nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa, kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea mjini Tunis, Tunisia.
Alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Palais Des Congres unapofanyika
mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa alipokelewa na Rais Kais Saied wa Tunisia.
Katika mkutano huo wa nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika,
Waziri Mkuu Majaliwa anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.