Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye amekimbizwa hospitalini mapema hii leo baada ya kuanguka ghafla akiwa kwenye shughuli zake za kawaida mkoani Tanga.
Habari kutoka mkoani humo zinasema kuwa Sumaye alipumzishwa kwa saa kadhaa katika hospitali hiyo ya Bombo na kupatiwa matibabu ya awali.
Madaktari wa hospitali hiyo wamesema kuwa baada kumpatia matibabu ya awali wamebaini kuwa alipatwa na shinikizo la juu la damu.
Baada ya kupatiwa matibabu hayo ya awali katika hospitali ya Bombo, Sumaye amesafirishwa kwa ndege kwenda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Ushauri wa Sumaye kupelekwa JKCI umetolewa na madaktari wa Bombo ambao wamesema kuwa huenda akawa na maradhi ya moyo.