Vijana wa mtaa wa Mnjaleni kata ya Magomeni manispaa ya Mtwara Mikindani wameelezea kufurahishwa na namna zoezi la sensa ya watu na makazi linavyoendeshwa, na hivyo kuwaomba vijana wenzao kuhakikisha wanahesabiwa.
Wakizungumza na mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Mtwara kwa nyakati tofauti, vijana hao ambao tayari wamehesabiwa wamesema maandalizi ya sensa ni mazuri kwa hiyo wasiiriki kikamilifu.
Wamesema zoezi hilo ni muhimu kwa kuwa litaisaidia serikali kufahamu idadi ya vijana nchini, na hivyo na kuweka mipango mizuri ya maendeleo kwa ajili yao.