Rais afanya uteuzi UDSM, NECTA

0
136

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu Damian Lubuva, ambaye amemaliza muda wake.

Pia amemteua Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Profesa Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 23 mwezi huu.