Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Hafla ya kupokea hati hizo za utambulisho imefanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodom.
Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais Samia.Suluhu Hassan kwa nyakati tofauti ni pamoja na balozi mteule wa Japan nchini Yasushi Misawa, balozi mteule wa Uganda nchini Kanali mstaafu Fred Mwesigye na balozi mteule wa Sweden hapa nchini Charlotta Ozaki Macias.
Wengine ni balozi mteule wa Kenya nchini Isaack Njenga Gatitu, balozi mteule wa Ubelgiji nchini Peter Hyghebaert na balozi mteule wa Afrika Kusini nchini Noluthando Mayende -Malepe.
Pamoja na kupokea hati hizo za utambulisho kutoka kwa mabalozi hao, Rais Samia Suluhu Hassan pia amefanya mazungumzo na mabalozi hao wateule kwa nyakati tofauti.