Mrema azikwa

0
135

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene, ameongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha TLP Augustino Mrema yaliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Kiraracha wilayani Moshi mkoa wa Kilimanjaro.


Akitoa salamu za serikali, Waziri Simbachawene amesema serikali haiwezi kusahau mchango mkubwa wa Mrema katika maendeleo ya demokrasia pamoja na maendeleo ya uchumi katika jamii.
Mrema alifariki dunia tarehe 21 mwezi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mkoani Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.