Biashara ya vitenge Kigoma yapungua

0
1139

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani  Kigoma  imetoa wito kwa wafanyabiashara wa kuuza vitenge mkoani humo kuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu za biashara yao.

Meneja wa TRA mkoani Kigoma, – Jacob Mtemang’ombe ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara wa vitendo mkoani humo kulalaikia kutozwa kodi kubwa pamoja na makadirio ya biashara yasiyoendana na uhalisia.

Ili kuhakikisha jambo hilo halijitokezi, Mtemang’ombe amewashauri wafanyabishara hao kutumia mashine za kutolea risiti za kielektroniki ambazo pia zitawasaidia kujua kiwango cha mapato na matumizi katika biashara zao.

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa  hapa nchini yenye historia ya wakazi wake kufanya biashara ya kuuza vitenge ambavyo wamekua wakivifuata katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Hata hivyo biashara hiyo ya kuuza vitenge imeanza kupungua mkoani Kigoma kwa madai ya wafanyabiashara kutopata faida kutokana na kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo ile ya  makadirio ya biashara yasiyoendana na uhalisia.