Dirisha la udahili JKT lafunguliwa

0
129

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limefungua dirisha la udahili kwa mafunzo ya jeshi ya kujitolea yatakayoanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena, ametoa wito kwa vijana wote wenye sifa za kujiunga na mafunzo hayo kuomba nafasi hizo kupitia ofisi za wakuu wa wilaya na ofisi za watendaji wa kata katika maeneo husika.

Amesema mafunzo yanayotolewa na JKT yanamuwezesha kijana kuwa mzalendo, kupata ujuzi wa aina mbalimbali wa kuzalisha mali pamoja na kujiajiri.

Aidha Brigedia Jenerali Mabena
amesisitiza kuwa JKT haijihusishi na kuajiri vijana hao ila zitakapotokea fursa kutoka katika taasisi za serikali na zisizo za serikali vijana hao wanaweza kupata fursa hizo watakapoonekana wana sifa.