Ndoa ya Rambo matatani

0
275

Mwigizaji wa filamu maarufu ulimwenguni Sylvester Stallone na mkewe Jennifer Flavin wameingia katika mgogoro ambao unaweza kusababisha ndoa yao iliyodumu kwa miaka 25 kuvunjika

Flavin (54) aliwasilisha ombi la kuvunjwa kwa ndoa na kutoka kwa nyota huyu mwenye umri wa miaka 76, Agosti 19 mwaka huu, katika mahakama ya Palm Beach County, mjini Florida.

“Ninaipenda familia yangu. Tunashughulikia masuala haya ya kibinafsi kwa amani na faragha,” Stallone aliambia moja ya chombo cha habari leo.

Wenza hao walifunga pingu za maisha mwaka 1997 baada ya kuishi takribani muongo mmoja katika uchumba.

Hata hivyo Stallon ambaye ni maaraufu kwa jina la Rambo na Mkewe Flavin wamefanikiwa kupata watoto wakike watatu ambao ni Sophia, 25, Sistine, 24 na Scarlet, 20.