Dar es Salaam kusaka mifuko ya plastiki

0
102

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameagiza kuanza kwa awamu nyingine katika mkoa huo ya operesheni ya kukamata mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kutumika nchini.

Operesheni hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 29 mwezi huu kwenye masoko yote ya mkoa wa Dar es Salaam.

Makalla ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi wa masoko yote ya mkoa wa Dar es Salaam, katika kikao kazi kilichojumuisha wakuu wa masoko, machinga na maafisa masoko.

Pia ameelekeza kufanyika msako wa kukamata viwanda bubu vinavyozalisha mifuko hiyo ya plastiki.