Katika kuhakisha zoezi la sensa ya watu na makazi linafanikiwa, Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoa wa Mtwara imewapa kazi ya ukarani wa sensa wasimamizi wa maudhui ya sensa, ili wananchi wengi zaidi waweze kuhesabiwa ndani ya muda uliopangwa.
Mratibu Msaidizi wa sensa ya watu na makazi mkoani Mtwara, Patrick Kyaruzi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la sensa linaloendelea.
Amesema uamuzi wa kuwapa kazi ya ukarani wa sensa wasimamizi wa maudhui ya sensa umefanyika baada ya baadhi ya wananchi kulalamika kutofikiwa kwa haraka na makarani hao wa sensa.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.