WhatsApp kuongeza kipengele kipya

0
256

Mtandao wa kijamii wa Whatsapp kupitia mmiliki wake Mark Zuckerberg, mapema mwaka huu ulitangaza kufanya maboresho katika siku za usoni, ambayo yataruhusu watumiaji wa mtandao huo kuunda vikundi vidogo ndani ya kundi kubwa.

Miezi kadhaa baada ya kutolewa kwa tangazo hilo na kipengele hicho kusubiriwa kwa hamu, hatimaye kitaanza kutumika kwa watumiaji wa “WhatsApp Beta”.

Kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka WABetaInfo, kipengele hicho sasa kinaonekana kwa watumiaji wanaotumia aplikesheni ya Whatsapp iliyohuishwa kufikia WhatsApp Beta v2.22.193 kwa wale wa Android.