Polisi kuhakikisha utulivu wakati wa sensa

0
746

Jeshi la Polisi nchini limewahakikishia watanzania kuwa limejiandaa ili kuhakikisha amani, utulivu na usalama vinakuwepo siku ya sensa ya watu na makazi itakayoanza usiku wa kuamkia Agosti 23 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime amesema, zimebaki saa chache kuanza kwa sensa ambapo kwa sasa hali ya usalama nchini ni shwari na itaimarishwa ipasavyo.

Misime amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapoona au kusikia viashiria vyovyote vyenye lengo la kukwamisha na kuleta dosari kwenye sensa, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.