Mizunguko wa pili Ligi Kuu watamatika

0
190

Mzunguko wa pili umetamatishwa Leo kwa michezo minne iliyochezwa katika viwanja vinne tofauti.

Mtibwa Sugar wamewalambisha Sukari wazee wa kupapasa Ruvu Shooting na sasa wamefikisha alama nne.

Polisi Tanzania na KMC wanaendelea kujikongoja baada ya wote kupoteza michezo yao ya awali na leo wamegawana alama moja moja kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Singida Big Star wao wanaendelea kuteleza kwenye barafu ambapo leo wamegawa dozi tena na sasa wamefikisha alama sita.

Geita Gold kagoma kuendeleza uteja kwa wakazi wa Dar ambapo leo kamng’ang’ania tajiri wa Chamazi Azam FC na kugawana alama moja moja.