Serikali kutolea ufafanuzi tozo miamala ya kielektroniki

0
179

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kumekuwa na upotoshaji kuhusu tozo ya miamala ya kielektroniki iliyoanza kutozwa mwaka huu wa fedha, na kwamba serikali itatoa ufafanuzi kuhusu madai ya baadhi ya watu kuwa tozo hizo zimeongezwa ama zimewekwa mpaka kwenye malipo ya mishahara ya watumishi wa umma na wa sekta binafsi.

Msigwa amewataka Wananchi kuwa watulivu kwa kuwa sio kweli kwamba tozo zimeongezwa, bali zilipunguzwa kwa asilimia 30 katika bajeti iliyopita na zimepunguzwa kwa asilimia 43 katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.