Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, umetunukiwa tuzo katika maonesho ya 15 ya sanaa yaliyofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 mwezi huu jijini Abuja.
Katika maonyesho hayo yaliyohusisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utalii na Uwekezaji, Tanzania imeshinda tuzo ya muonyeshaji bora katika masoko ya mtandaoni (E. Marketing).