Waziri wa zamani wa Uchukuzi William Kusila amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mkoani Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Wakati wa uhai wake, Kusila amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma.
Nafasi nyingine ni waziri wa Kilimo, mkuu wa mkoa wa Dodoma na mbunge wa jimbo la Bahi mkoani Dodoma.