Kampuni ya Google kupitia mtandao wa Youtube umepanga kuanza kuweka alama “Watermark” kwenye video ambazo zinachezwa kwenye mtandao huo katika siku za hivi karibuni.
Hatua hiyo ya YouTube inakuja baada ya kampuni ya China ya TikTok kufanya vizuri katika mtindo wa video zake fupi ambazo huwa zikichezwa na alama maalumu ya mtandao huo ikionekana katika kila video.
Katika ukurasa wa Google, Meneja wa YouTube, Sarah ameandika “kipengele kipya cha watermark kitazinduliwa kwa ajili ya kompyuta ya mezani wiki chache zijazo”.
Yotube imepanga kuanza kutumia alama hiyo kwenye video ambazo zitachezwa kwenye kompyuta za mezani na endapo mambo yatakua sawa basi huduma hiyo itazinduliwa pia katika simu za mkononi