Umeme warejea baada ya kukatika nchi nzima

0
171

Nishati ya umeme imerejea nchini Nigeria, baada ya nchi nzima kukosa umeme kufuatia mgomo ulioitishwa na wafanyakazi wa sekta ya umeme.

Huduma hiyo imerejea kufuatia mazungumzo kati ya chama cha wafanyakazi wa sekta ya umeme nchini Nigeria na serikali.

Kwa siku ya jana, nchi nzima ilikosa umeme baada ya wafanyakazi hao kuzima gridi ya Taifa wakishinikiza nyongeza ya mishahara.

Wafanyakazi hao wa sekta ya umeme nchini Nigeria wanailaumu serikali kwa kupuuza madai yao ya muda mrefu ya kuwapatia nyongeza ya mishahara.

Wafanyakazi hao wametishia kufanya tena mgomo utakaodumu kwa muda wa wiki mbili, endapo madai yao hayatashughulikiwa.