Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Binilith Mahenge, mkuu wa mkoa wa Singida mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Dkt. Mahenge anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Longinus Rutasitara ambaye alimaliza muda wake.
Pia Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Aurelia Kamuzora wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Profesa Kamuzora anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Festus Limbu ambaye alimaliza muda wake.
Uteuzi huo ni kuanzia tarehe 11 mwezi huu.