Uhesabuji kura waingia siku ya tatu

0
244

Raia wa Kenya bado wako kwenye shauku ya kutaka kujua Rais wa awamu ya tano wa nchi hiyo ni nani, huku zoezi la kuhesabu kura likiingia siku ya tatu.

Tume ya uchaguzi na mipaka ya Kenya (IEBC) nchini humo inaendelea kuhakiki fomu za matokeo katika kituo kikuu kilichopo jijini Nairobi.

Matokeo ya awali yanaonesha mchuano mkali kati Dkt. William Ruto na Raila Odinga.

Ili kupata mshindi, mgombea anatakiwa kupata 50%+1 ya kura zote halali na walau 25% ya kura halali kutoka kwenye kauti 24 kati ya kaunti 47 zilizopo.