Raila aongoza kura za Urais

0
286

Matokeo ya uchaguzi yanaendelea kutolewa nchini Kenya kufuatia uchaguzi uliofanyika Agosti 9, 2022.

Kwa upande wa matokeo ya kura za Urais bado wagombea wawili ambao ni Raila Odinga kutoka muungano wa Azimio la Umoja na William Ruto kutoka muungano wa Kenya Kwanza wanachuana.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Nation, matokeo ya awali yaliyotolewa hadi kufikia saa moja asubuhi hii,  Raila anaongoza kwa kupata kura 5,216, 932 ambazo ni sawa na asilimia 51.83 ya kura zote zilizopigwa.

Ruto yeye ana kura 4,782,682 ambazo ni sawa na asilimia 47.51.

Matokeo hayo ya awali ni kutoka katika vituo 31, 607 vya kupigia kura,  kati ya vituo 46,229

Habari zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa, hali imeendelea kuwa shwari katika maeneo mengi nchini humo wakati matokeo rasmi yakisubiriwa.

Kwa matokeo ya kura za Urais nchini Kenya fuatilia https://elections.nation.africa/